Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa leo amezindua kitabu cha kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Uzinduzi huo Umefanyika katika Hotel ya Eden jijini Mbeya chini ya taasisi inayoziunganisha taasisi za dini nchini TIP.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kukemea vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii na kuhimiza juu maadili.
Aidha, ameipongeza TIP kwa jitihada za kuandaa kitabu hicho kinachokemea vitendo hivyo
Pia DC Malisa amepongeza mchango wa wadau kama vile UNICEF na UNFPA kwa kuwa, imara kupingana na vitendo vya unyanyasaji katika jamii.
DC Malisa amesisitiza wadau kupeleka elimu ya maadili shuleni na katika ngazi za familia ili jamii ipate kunufaika na elimu ya maadili.