Home KITAIFA DAWASA KUTUMIA BILIONI 424 KUTEKELEZA MIRADI 7 YA HUDUMA YA MAJISAFI

DAWASA KUTUMIA BILIONI 424 KUTEKELEZA MIRADI 7 YA HUDUMA YA MAJISAFI

 

MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dar es-Salaam (DAWASA) imejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati saba ikiwemo mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji na mradi wa maji Kwala ambapo miradi yote itagharimu jumla ya Shilingi bilioni 425.9.

 

Hayo yameelezwa leo Agosti 11 jijini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo,Kiula Kingu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu yake na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2023/2024 .

“Ukamilishwaji wa miradi ya kimkakati na miradi midogo midogo ya kusogeza huduma kwa wananchi imewezesha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kufikia zaidi ya wakazi 700,000 ambao hapo awali hawakuwa na huduma bora za majisafi kwa mwaka 2022/23,”

Amesema DAWASA imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo yakuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi ya lita 780,000 za majitaka zitakuwa zikichakatwa kwa siku.

“Miradi hii ambayo pia itajumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30, itasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hizi muhimu na hivyo kuboresha usafi wa mazingira”amesema

Kingu ameendelea kwa kusema DAWASA imejipanga kikamilifu kuchukua hatua za makusudi za kuboresha usafi wa mazingira kupitia miradi mikubwa na midogo kwasababu upatikanaji wa maji unapoongezeka unapaswa uambatane na usimamizi madhubuti wa usafi wa mazingira.

“Upatikanaji wa maji unapoongezeka unapaswa uambatane na usimamizi madhubuti wa usafi wa mazingira na Katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala, miradi ya kuchakata majitaka itajengwa maeneo ya Mbezi Beach na Buguruni, Mradi wa Mbezi Beach unatekelezwa kwa ushirikiano kati yaSerikali na Benki ya Dunia ambapo jumla ya shilingi bilioni 132.3 zitatumika kujenga mtambo wa kisasa wenye uwezo wa kuchakata lita milioni 16 kwa siku.”

Previous articlePROF. KATUNDU: BIL.3 ZAKOPESHWA KUWEZESHA MIRADI YA VIJANA
Next articleSAFARI YA WACHIMBAJI NCHINI CHINA KULETA TIJA – DKT. KIRUSWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here