Home KITAIFA DAWA NYINGI ZINAZOSAMBAZWA NA MSD HAZITOKI TANZANIA -MBUNGE SHANGAZI

DAWA NYINGI ZINAZOSAMBAZWA NA MSD HAZITOKI TANZANIA -MBUNGE SHANGAZI

‘’Bado kuna maeneo mengi ya kiuchumi ambayo hatujayatumia vizuri kama taifa,hizi nchi tunazozingumzia hapa ukiacha nchi mbili Afrika kusini na Angola zote hizi nyingine zote GDP capital pato la taifa tunawazidi kwa maana sisi uchumi wetu upo juu zaidi,’’

‘’Suala zima la afya katika usamabazaji wa madawa nahapa nataka niweke wazi kwamba hata MSD waliwahi kupata zabuni ya kusambaza dawa katika nchi zte za SADC wakati huo zikiwa 13 sasa zimefika 16 sasa ninawaomba tunaweza kuishirikisha pia vyema wizara ya afya kupitia MSD Kwenda kutumia fursa hiyo yakusambaza madawa katika hizo nchi, imeonekana kabisa usambazaji wa dawa unaofanywa na MSD ndani ya Tanzania ni usambazaji wa kimataifa’’

‘’Suala lingine ninalotaka kushauri suala zima la ukuzaji wa lugha ya kiswahili, hapa napo ni lazima tuwe na mkakati madhubuti kiswahili hichi tunachozungumza leo siyo chakwenda kufundishia ni lazima tujipange upya bakta na wizara inayohusika tuanze kuandaa waatalamu ambao watakwenda kufundisha hicho kiswahili katika nchi ambazo tunakusudia, haitawezekana kudundisha kiswahili kama huwezi ukajua lugha yake ya nchi hiyo zipo nchi zinazungumza kireno , kwahiyo ni lazima tuandae watu wetu wa kwenda kufundisha kiswahili hicho wawe wanakijua ili waweze kurahisisha uwasilishaji,’’

Hayo yamesemwa agosti 31, 2023 bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi Wakati akichangia azimio la Bunge kuhusu mapenekezo ya kuridhia itifaki ya biasahara ya huduma ya jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa afrika ya mwaka 2012(SADC PROTOCOL ON TRADE IN SERVICES,2012)

Previous article“WATOTO WAPELEKWE JANDO LA ZAMANI NA SI LA KISASA ILI WAKIOA WAJUE CHANGAMOTO ZA NDOA” _GWAJIMA
Next articleWANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EL-NINO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here