Home KITAIFA DAVID SILVA ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KULIPWA BAADA YA KUPATA MAJERAHA

DAVID SILVA ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KULIPWA BAADA YA KUPATA MAJERAHA

Mchezaji wa zamani wa machester city David Silva ametangaza kustaafu soka la kulipwa baada ya kupata majeraha,Silva amecheza mechi 436 Zaidi ya miaka 10.

Tangu aondoke kwenye uwanja wa Etihad mwaka 2020 mhispania huyo amekuwa akicheza kwenye klabu ya Real sociedad, kiungo huyo mkongwe amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kilichomaliza kwenye nafasi ya 4 kwenye ligi ya hisipania ikiitwa Laliga msimu wa 2022/23 na klabu hiyo kurejea kucheza hatua ya makundi klabu bingwa ulaya baada ya muongo mmoja.

Majeraha ya Silva ameyapata wakati wakijiandaa na msimu mpya wa 2023/24 na amestaafu akiwa na miaka 37.Katika chapisho la mtandao wa kijamii wa twitter Silva alichapisha video akisema “Ni wakati wa kusema kwaheri kwa kile ambacho nimejitolea kwenye maisha yangu yote,”

Previous articleVYUMBA VYA MADARASA YA BOOST BUNDA DC VYAMKOSHA RC MTANDA
Next articleBENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUTEKELEZA MASUALA YA JINSIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here