Home KITAIFA DAS MPYA SAME ASISITIZA USHIRIKIANO

DAS MPYA SAME ASISITIZA USHIRIKIANO

 

Katibu Tawala wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Upendo Wella amewaomba wakazi wa Same wakiwemo pia watumishi wa umma na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuendeleza ushirikiano kuwa na urahisi katika uwajibikaji na kufanikisha adhma ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na serikali yake kuleta maendeleo.

Ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa katibu tawala wa Wilaya hiyo Sospeter Magiera aliye hamishiwa Wilaya ya Hai mkoa huo wa Kilimanjaro katika mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassani.

Katibu tawala huyo Upendo Wella amesema ushirikiano kwenye utendaji ndio njia pekee na rahisi kwa kila mmoja kufanikisha wajibu wake.

“Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia wananchi wa Same hasa kutatua migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na wote tuwe kitu kimoja ili tuendelee kukuza Uchumi wa Taifa letu”.

Kwa upande wake Sospeter Magonera aliyekuwa katibu tawala wa Wilaya hiyo ambae kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Same, amewashukuru watumishi na wakazi wote wa Same kwa ushirikiano katika kipindi chote cha utumushi wake kwenye Wilaya hiyo huku akisema kwakua lengo la serikali ni kujenga nchi na kuleta maendeleo, ushirikiano ndio msingi wa kufanikisha mipango hiyo.

Previous articleRAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KUTANGULIZA UZALENDO NA KUILINDA MIRADI
Next articleSIMBACHAWENE AKIRI MAPUNGUFU SHERIA LIKIZO YA UZAZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here