Home KITAIFA DARAJA MTO NKANA MOMBA LINAHITAJI KUJENGWA KUWANUSURU WANANCHI

DARAJA MTO NKANA MOMBA LINAHITAJI KUJENGWA KUWANUSURU WANANCHI

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Mchungaji  Peter Msigwa akiwa kwenye ziara ya chama hiko katika Kata ya Chitete Wilaya ya Momba Mkoani Songwe, ambapo amelazimika kutumia Mtumbwi kuvuka Mto Nkana baada ya kushindwa kuvuka kwa kutumia usafiri wa Gari.

Mto huo (Nkana) unaunganisha Vijiji vya Chindi na Msangano ambapo mto huo hauna Daraja tangu nchi kupata Uhuru hivyo ni vema Serikali ikatupia jicho la tatu kujenga Daraja ili kuwanusuru wananchi na madhira mbalimbali.

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Peter Msigwa, anaendelea na ziara ya kichama Mkoani Songwe baada ya kutoka Jimbo la Lupa Chunya ikiwemo kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Previous articleMATANKI YA KUBEBA MAFUTA YA NCHI ZA RWANDA, BURUNDI, MALAWI NA CONGO UHAKIKIWA NA WAKALA WA VIPIMO WMA WA MISUGUSUGU KIBAHA MKOANI PWANI
Next articleMITAMBO ILIYOZINDULIWA NA RAIS DKT. SAMIA YAANZA UCHOROGAJI NYAMONGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here