Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kushirikiana na kituo cha afya cha chuo hicho kimeandaa bonanza maalumu la afya katika kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kujilinda dhidi ya magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kupitia michezo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe upande wa taaluma Eliza Mwakasengula, amesema lengo la bonanza hilo ni kuwatengenezea wafanyakazi utamaduni wa kupenda kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara.
Bonanza hilo limehusisha wafanyakazi mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha SUA, timu kutoka Kihonda Vterans na timu ya mchezo wa mpira wa kikapu Bwalo la Umwema.