Home KITAIFA CHUO CHA (MUM) CHAFANYA MDAHALO KUJADILI SUALA LA MMOMONYOKO WA MAADILI

CHUO CHA (MUM) CHAFANYA MDAHALO KUJADILI SUALA LA MMOMONYOKO WA MAADILI

Katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Chuo Kikuu cha Waislam (MUM) kimefanya mdahalo na wadau mbalimbali kujadili suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii na namna ya kupata ufumbuzi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo huo ulioshirikisha wadau mbalimbali mkoani Morogoro, Makamu mkuu wa Chuo cha MUM, Prof. Hamza Njozi amesema kuwa harakati za maisha kwa wazazi zimechangia watoto kuharibika kutokana na kukosa muda wa kuzungumza nao.

Amesema kuwa ipo haja sasa wazazi kukaa kwa pamoja na watoto wao na kuwalea kwa misingi ya dini ili kuweza kurejesha maadili mema yaliyokuwepo hapo awali.

Naye Mkuu wa kitengo cha dawati la Jinsia Mkoa wa Morogoro Dkt. Mwanaidi Lwena amesema kuwa watoto kutipelekwa katika vituo vya malezi ya kiimani ikiwa ni pamoja na madrasa kumechangia watoto wengi kuharibika kimaadili.

Previous articleRAS SENEDA ATAKA MFUMO WA M-MAMA UDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO
Next articleHATIMAYE NDOTO YA MTOTO HAMIMU YA KUKUTANA NA RAIS SAMIA YATIMIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here