Home KITAIFA CHUO CHA AFA FASHION ACADEMY CHAJA NA JUKWAA LA KUIBUA VIPAJI VYA...

CHUO CHA AFA FASHION ACADEMY CHAJA NA JUKWAA LA KUIBUA VIPAJI VYA WABUNIFU WA MITINDO

 

Na Joel Maduka Dar es Salaam.

Katika kutambua juhudi za wabunifu wa mitindo na mavazi ,Chuo cha AFA Fashion Academy kimeamua kuja na jukwaa la kuibua vipaji vya wabunifu mitindo ambapo Washiriki wa jukwaa hilo ni wanafunzi wa Chuo hicho waliohitimu mafunzo na wamepata weledi wa kubuni mitindo ya kisasa.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa AFA Fashion Academy na Anna Collection Bi Anna Peter Lunguya amesema lengo la jukwaa hilo ni kuendelea kuongeza thamani ya ubunifu mitindo na namna ya kutengeneza pesa kupitia sanaa hiyo..

“Wazo la kufungua chuo lilikuja kwa lengo la kutaka kuona tunaimalisha na kuwajengea uwezo watu wengine kupitia vipaji vya ubunifu waweze kutengeneza Fedha tunaona kila siku serikali yetu imekuwa ikisisitiza kwa vijana kujiajiri hivyo ubunifu wa mitindo ni moja ya ajira kubwa sanaa kwa vijana” Anna Peter Lunguya Mkurugenzi wa AFA Fashion Academy.

 

Pia ameeleza kwa namna ambavyo alipata ushawishi wa kufikia malengo yake kupitia mbunifu mbobezi Kasikana, Precious Mwalimu wa Mitindo kutoka Nigeria na Dorina mbunifu wa mavazi kutoka Kenya,ambapo kwa Pamoja amejumuisha wabunifu hao kwenye jopo la majaji ambao watakagua na kutoa viwango katika kazi zilizobuniwa na wanafunzi hao na hatimaye watatangaza washindi katika aina tatu za mavazi yatakayopitishwa kwenye jukwaa la ubunifu.

 

Kwa upande wake mbunifu wa mitindo na mavazi kutoka Mkoani Geita Kasikana Joseph alisema yeye kama jaji na japo la majaji wengine watakuwa tayari kutenda haki kwa kutoa kura sawa pamoja na kuwatangaza washindi sahihi wa mitindo na ubunifu.

 

Wengine walioambatana na jopo la majaji ni Wabunifu mshuhuli wa mitindo na mavazi Martin Kadinda na Stephen Designer wa brand ya Neste Fashion.

 

Aidha katika kuelekea kilele cha kutangaza wabunifu Bora chipukizi wa mitindo na mavazi kutakuwa na semina ya wafanyabiashara wa mitindo ambayo itaongozwa na Precious Tonna Mwalimu wa mitindo kutoka Nigeria, pamoja na wabobezi wengine .

Previous articleWAZIRI AAGIZA UCHUNGUZI MADHARA KUHUSU ‘ENERGY” : MAGAZETINI LEO JUMANNE APRILI 25/2023
Next articleMTOTO ALIVYOWATOROKA WAZAZI USIKU KUMFUATA RAIS SAMIA KUOKOA MAISHA YAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here