Chama cha wavuvi Tanzania kimeipongeza Serikali kuwatafuta wawekezaji kwajili ya kuwekeza katika Bandari ya Dar es salaam ambayo imekuwa ikilalamikiwa sana na watanzania pamoja na watumiaji wake kwa kuchelewesha mizigo na kusababisha baadhi ya wafanyabiashara kutumia bandari za nchi jirani kitendo kinachopoteza mapato.
“ Kampuni ya Dp world ni kampuni kubwa duniani na nchi nyingi zingependa kufanya nayo kazi sizani kama wao ndio wametutafuta naamini sisi ndio tumewatafuta ili kuleta ufanisi katika bandari zetu na kuondoa ujanja ujanja na ucheleweshaji wa mizigo na kusababisha hasara kwa baadhi ya wafanyabiasha,Bakari Kadabi Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi Tanzania Bakari Kadabi,ameiomba Serikali kuweka kwa uwazi mikataba yake na kampuni ya Dp world nini kiki kiukwa kinapelekea kuvunjika kwa mkataba huo huku akiwahasa wanasiasa wajiepushe na Utanganyika na Uzanzibar ambayo ni hatari na yanaweza kupelekea mpasuko kwa Taifa.
“ Ikumbukwe wabunge wetu walienda kujifunza kwa kutumia pesa za watanzania,niseme umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kazi iendelee Rais wetu Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan pia tunaomba wavuvi wa Ziwa Victoria tujengewe bandari ya wavuvi ya kufikishia samaki, kabla ya kupeleka kwenye masoko ili kuzipa thamani na ushindani sokoni, Bakari Kadabi Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi Tanzania.
“ hivyo kwa uwekezaji huo tunaenda kuunganisha mifumo ya uwekezaji wa kisasa na Reli yetu ambayo itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa pia daraja letu la JPM Magufuli maarufu Kigongo – Busisi likishakamilika na uchumi wa maziwa makuu utainuka kwa kasi kubwa pia nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania tusiamini kwamba kila mikataba inayofungwa na viongozi wetu ndani yake kuna dalili za rushwa, amesisita Kadabi.