KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa mwenendo wa Ligi Kuu, iliyochini ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 19,2023 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo.
Ligi kuu ya NBC Mechi Namba 222:
Simba Sc 3 vs 0 Ruvu Shooting Fc
Mchezaji wa klabu ya Simba Clouts Chama amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh.500,000 (Laki tano) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezeji wa Klabu ya Ruvu Shooting, Abal Kassim Suleiman,tukio hilo lilitokea katika mechi iliyochezwa Mei 12,2023 mwenye dimba la Azam Complex.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.