Home KITAIFA CHADEMA NYASA YAHIMIZA KATIBA MPYA, KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI, MAENDELEO YA WATU

CHADEMA NYASA YAHIMIZA KATIBA MPYA, KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI, MAENDELEO YA WATU

NA JOSEA SINKALA, ILEJE SONGWE

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa Gwamaka Mbughi, amekemea chuki za kisiasa anazosema zinaendelea katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe na kueleza kwamba siasa sio ugomvi.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ikumbilo kata ya Chitete kwenye mkutano wa hadhara wilayani Ileje.

“Mimi ninao marafiki wa CCM nina hudhuria kwenye misiba kwenye harusi, ninapokuwa na shughuli zangu watu wa CCM wanakuja wasio na vyama wanakuja kwanini tubaguane kwenye shughuli za misiba, kwanini mtu mmoja anapandikiza chuki kwenye kijiji chetu (Ikumbilo) kwenye Kata yetu ya Chitete, tusio na vyama, tulioko CHADEMA, tulioko CCM tukatae hawa wanaopandikiza chuki ya kisiasa ya kutubagua katika shughuli mbalimbali za kijamii”, Gwamaka Mbughi, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa.

Aidha Gwamaka ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kwamba kumekuwa ubadhirifu wa fedha za Umma kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu CAG.

Katibu Gwamaka Mbughi amesema Serikali imekuwa chanzo cha ubadhirifu wa fedha za Umma kutokana na kutowachukulia hatua za kisheria wanaohujumu fedha na mali za umma akisema Katiba mpya itakuwa suluhu ya kuleta nidhamu na uwajibikaji kwa wananchi na viongozi na kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.

“Kwa mujibu wa ripoti ya CAG Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ilikusanya Fedha za ndani Bilioni moja milioni mia saba themanini na saba laki sita sitini na nane, fedha zilizopitishwa na Halmashauri zilikuwa ni ndogo kuliko fedha zilizokusanywa kwa wananchi” , ameeleza Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Gwamaka Mbughi.

Amesema Katiba mpya ni sasa ili mamlaka makubwa yawe kwa wananchi ambao ndio waendeshaji wa Taifa lao hivyo kuitaka Serikali na wadau kuamka sasa kwa kuruhusu kwa vitendo mchakato wa Katiba mpya kabla ya chaguzi za 2024/2025.

Previous articleSAFARI ZA MWENDOKASI MBAGALA LEO RASMI
Next articleWAKALA WA MELI TANZANIA WAUNGA MKONO UJIO WA DP WORLD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here