Home SIASA “CHADEMA KUWENI NA SHUKRANI”-KINANA

“CHADEMA KUWENI NA SHUKRANI”-KINANA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka vyama vya upinzani nchini kuwa waungwana na wenye shukrani kwani Rais Samia amefanya mambo mengi mazuri hivyo anastahili kuheshimiwa.

Akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora, Kinana amesema;

“Walikuwa hawajapokea ruzuku yao tulipo Kutana na Rais na wao, wakasema sasa tunaona tumeelewana tunaomba ruzuku yetu tuichukue na mtupe ruzuku yetu tangu uchaguzi ulipomalizika, Rais akasema sawa andikeni barua, wameandika ruzuku yao wakalipwa lakini matokeo yake unaambiwa Rais huyu hana maana Dooh!!”

” Nimekupa hela zako sina maana , nimekufungulia mikutano akili za matope, lakini Rais ni binadamu inataka moyo wa uvumilivu sana mtu kuweza kuvumilia mambo yote haya, ukiangalia mamlaka aliyonayo Rais lakini akasema hapana nimewasikia nitaendelea na kazi yangu Watanzania ni waungwana wataelewa jambo hili vizuri zaidi ya wanavyolieleza wao wapinzani” Kinana

Kinana ameendelea kuwasihi upinzani kuacha kejeli dharau na matusi kwani havisaidi kuletea maendeleo;

“Niwasihi matusi kejeli ,dharau , kupuuza hakusaidi sana… Sisi tumekaa nao tumewaheshimu , tumewasikiliza, kikao cha mwisho na wao tulifanya mwezi Juni hakuna agenda hata moja imetoka CCM zote zimetoka kwao na nyingi tumezifanyia kazi, walikuwa na wanachama wao walikuwa na kesi nyingi tu zote zimefuatiliwa kwa utaratibu husika nyingi zimefutwa zimebaki mbili tu na hizo mbili ni kwa sababu zinahusika na mauaji huwezi zifuta haraka haraka…. Basi jamani yote haya hayafai? haya stahili kushukuriwa? haya stahili Rais kuheshimiwa?”_

“Tumefungua mikutano kujakusemwa , kusakamwa na kuzalilishwa, tumetoa ruzuku walioomba kusafiria kupata fursa yakutusema na kututukana, watu walikuwa wamefungwa wameachiliwa atusemi tumewafanyia hisani lakini tumekuwa waungwana, Rais amekuwa muungwana sana”_ Alisisitiza Kinana

Aidha Kinana amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuimarisha umoja na mshikamano na kutokutumika vibaya uhuru waliopewa.

“Watanzania tuimarishe umoja na mshikamano ,tupokee kwa mikono miwili utaratibu huu wa maridhiano ambao Rais ameuridhia kwa kupenda kuleta amani na umoja katika nchi yetu, tusiutumie vibaya, usifikiri kwa kutukana, kwa kukejeli, kwa kuonyesha dharau hoja yako itakubalika kwa haraka hoja yako itatupiliwa mbali, peleka hoja yako kistaarabu itakubalika ” _Alisema Kinana

Pamoja na yote Kinana amewasihi wapinzani kuwa waungwana na wajenge hoja kwa kujibu hoja na sio kujenge hoja kwa dharau.

Previous articleCCM, CHADEMA SASA JINO KWA JINO ….WANYUKANA MIKOANI SAKATA LA BANDARI, LISSU ATOA UTABIRI UCHAGUZI MKUU 2025_ MAGAZETINI LEO JUMATATU JULAI 31/2023
Next articleUSHIRIKINA ULIMCHUKUA MTOTO WANGU, DAWA HII IMENISAIDIA KUMPATA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here