Home KITAIFA CHADEMA KATAVI YAHIMIZA MAANDAMANO JUMA LIJALO

CHADEMA KATAVI YAHIMIZA MAANDAMANO JUMA LIJALO

KATAVI

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi Roda Kunchela, amewataka wananchi ndani na nje ya mkoa huo kuungana na chama hiko kufanya maandamano ya kushinikiza kutosainiwa kwa miswada mitatu ikiwemo ya Tume ya Taifa Uchaguzi na kupatikana kwa katiba mpya.

Mwenyekiti huyo amesema hayo akiwa katika ofisi ya CHADEMA mkoani humo kufuatia agizo la Chama hiko Taifa kwa viongozi wa ngazi za chini kuratibu kufanyika kwa maandamano hayo ambayo ni haki yao kikatiba.

Roda, amesema agizo la mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe la kufanya maandamano ya amani nchi nzima ni takwa la kikatiba kwa mstakabali wa kudai haki ya maoni ya wananchi kuheshimiwa badala ya nchi kuendeshwa kwa matakwa na maslahi ya wachache.

Amewatolea wito wananchi wote kuungana ili kupinga mwenendo anaosema ni mbovu katika kuendesha Taifa na kukosa dira ya maendeleo ya kweli kwa kutokuwa na katiba bora inayoendana na wakati na yenye kuheshimu haki za watu.

“CHADEMA tumepeleka maombi yetu lakini yametupiliwa mbali, ninyi (wananchi) mnafahamu kuwa tuna uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji mwaka huu (2024) na Uchaguzi mkuu 2025 lakini hawa wakurugenzi ambao ni wateule wa Rais ndio wasimamizi ina maana wakiamua hatuwezi kupata viongozi bora sasa haya ndio miongoni mwa mambo yanayotufanya tuingie barabarani”, ameeleza Roda Kunchela, mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi.

Kufuatia madai yake hayo na mengineyo, Roda amewaomba wananchi kushiriki katika maandamano ya amani yatakayofanyika tarehe Januari 24,2024 jijini Dar es Salaam.

Previous articleWAZIRI BASHUNGWA: WAKANDARASI WABABAISHAJI KUCHUKULIWA HATUA
Next articleZIARA YA WAZIRI WA UCHUKUZI INDIA YAONGEZA MATUMANI ZAIDI KATIKA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here