Home KITAIFA CGP NYAMKA ASISITIZA NIDHAMU KWA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA

CGP NYAMKA ASISITIZA NIDHAMU KWA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhani Nyamka ameendelea na ziara yake ya kikazi Mkoa wa Ruvuma kwa kuongea na Maafisa na askari wa Magereza Mkoa Ruvuma,Gereza Tunduru na Gereza Wilaya Songea.

Pamoja na mambo mengine CGP.Nyamka amesisitiza nidhamu, upendo, ushirikiano, umoja, kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande mwingine CGP. Nyamka ametoa wito kwa askari wote kujiunga na mfuko wa kutatua matatizo ya dharura katika vituo vyote Tanzania bara.

Pia CGP.Nyamka alipata fursa ya kuongea na wafungwa na mahabusu na kusikiliza shida zao ikiwemo swala la wafungwa wa kigeni kutoka nchini Ethiopia, changamoto ya sare za wafungwa.

Akisoma taarifa ya Magereza Mkoa Ruvuma,Mkuu wa Magereza Mkoa huo(RPO) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Silvester Mrema amemuomba Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhani Nyamka kujengwa gereza katika Wilaya ya Namtumbo ili kupunguza msongamano katika Gereza Wilaya Songea.

Akisoma taarifa ya Gereza Wilaya Tunduru Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu wa Magereza (SP) Uswege W. Yoram amemshukuru CGP. Nyamka kwa kutembelea kituoni hapo kusikiliza na kutatua changamoto zinazo wakabili katika kituo hicho ikiwemo upungufu na uchakavu wa magodoro kwa wafungwa na mahabusu.

Hata CGP. Nyamka amehitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma,kwa kuhaidi kwenda kuzitatua changamoto zote walizompatia na kuzipatia suluhu

Previous articleWAZIRI MKUU: SERIKALI INATAKA KUONA WANANCHI WAKIPATIWA HUDUMA ZA AFYA KOKOTE WALIPO
Next articleSHILINGI BILIONI 25 ZATENGWA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here