Home SIASA CCM YAAGIZA MCHAKATO WA BANDARI UHARAKISHWE KUKIMBILIA MAENDELEO, SILINDE APIGILIA MSUMARI

CCM YAAGIZA MCHAKATO WA BANDARI UHARAKISHWE KUKIMBILIA MAENDELEO, SILINDE APIGILIA MSUMARI

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Naibu Waziri wa Mifugo Mhe. David Ernest Silinde amesema Uwekezaji wa Bandari ni mpango unaokwenda kuongeza mapato ya nchi na kwamba ili Taifa lolote liendelee kwa kasi ni lazima lijiimarishe kwenye Sekta ya uwekezaji badala ya kutegemea kodi za wananchi pekee.

Naibu Waziri Silinde ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tunduma amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jijini Mbeya mbele ya Katibu mkuu wa CCM Danieli Chongolo.

Amesema uwekezaji wa Bandari ni mzuri na unakwenda kupanua wigo wa upatikanaji fedha ikiwemo kwenye Wizara ya mifugo na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyopambana kuiongoza nchi kwa mafanikio mengi katika kada mbalimbali.

Akizungumza mkutanoni hapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Danieli Chongolo amesema suala la uwekezaji wa Bandari ni la Chama hicho tawala hivyo kuiagiza Serikali kuharakisha mchakato wa pili ili kuingia mkataba na Kampuni ya DP World baada ya kumalizika kwa hatua ya makubaliano na kampuni hiyo.

Pia ameitoa hofu jamii kuwa mkataba huo hautakuwa na shida hivyo wasiyumbishwe na kelele za watu anaosema wana maslahi yao binafsi.

“Suala la Bandari ni letu (CCM) tukicheka na wanaopotosha adhabu itakuwa ni ya kwetu. Ilani ya CCM ndio imebeba matumaini ya watanzania, sasa hivi ukipita kila mahali unaona barabara zinachimbuliwa kwasababu tuliahidi kwenye ilani”, Danieli Chongolo,katibu mkuu CCM.

“Jamaa zetu (wapinzani wa bandari) wamepita na kusukumasukuma uongo juu ya Bandari yetu. Na Serikali yetu tumeipa kazi sasa hivi, hatuna mkataba wa uendeshaji na nchi yoyote na bandari yoyote tuagize sasa Serikali chakateni haraka kwenda kwenye mkataba wenyewe”, Katibu Mkuu Danieli Chongolo akizungumza jijini Mbeya.

“Ngoja niwaambie Bandari zote hapa nchini zinaingiza kwa mwaka Sh. Bil.795.226 lakini wao (TPA) wanatumia asilimia 99 ya hizo hela, hapa kuna genge la watu wana mlo lazima wachonge mdomo wanapoona mambo yanabadilika. Kwahiyo niwaambie wana CCM wenzangu msibabaishewe, agenda hii ni ya CCM tutafanikiwa”, Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo.

“Mimi ni mtu wa Nyanda za juu kusini, Iringa na Njombe ndio nyumbani, Siwezi-simama hapa nikatetea jambo ambalo sioni kwamba lina tija kwa watu wangu. Kwenye hili (Uwekezaji wa Bandari) CCM tumeamua haturudi nyuma na naagiza Serikali ichakate haraka twende mbele wasitucheleweshe na niwahakikishie maoni yenu yote ya msingi tutahakikisha yanachukuliwa na kuingizwa kwenye mkataba wa Bandari”, Katibu Mkuu wa CCM Danieli Chongolo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya Dkt. Stephen Mwakajumilo, amewataka wa-Tanzania kuungana bila kujali itikadi zao katika suala la maendeleo badala ya kuendekeza malumbano yasiyo na tija ikiwemo kwenye suala la Bandari analosema yeye binafsi na CCM wanaamini ni jambo sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Naye Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Stephen Masatu Wassira amesema kama mmoja ya wapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar hawezikuona raslimali za Taifa zikichezewa hivyo kuwataka wananchi kupuuza maneno kwamba Bandari ya Dar es Salaam imeuzwa akisema bandari na raslimali nyingine zitaendelea kuwa salama.

Previous articleUTENDAJI POLISI WAMKERA RAIS ATAKA IJITATHMINI _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI JULAI 16/2023
Next articleMAKAMBA AYATAKA MAKAMPUNI YA BIMA NCHINI KUTUMIA FURSA KATIKA SEKTA YA NISHATI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here