Chama cha mapinduzi CCM wiayani Ileje mkoani Songwe kimewataka makatibu wa siasa na uenezi kuzingatia itifaki katika Kutekeleza majukumu yao.
Hayo yamebainishwa na katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ileje Maoni Jeckisoni Mbuba wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo makatibu hao wa siasa na uenezi ngazi ya kata kutoka kata 8 za wilaya hiyo.
Mbuba amesema lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi hao hasa ikizingatiwa uchaguzi umefanyika mwaka jana hivyo wengi wao wanakumbushwa majukumu yao.
Mbuba amesema mafunzo hayo yanatoa dira ya uzalendo kwenye chama kutambua majukumu Yao ndani ya chama.
“Viongozi wenzangu nawasihi mafunzo mliyoyapata itumieni Kwa kuwa wazalendo na elimu hii mkaieneze ngazi ya matawi lengo ni kuhakikisha Wanaccm wanakuwa imara kuelekea uchaguzi serikali za mitaa”, amesema Mbuba.
Aidha Mbuba amesema kazi ya uenezi si ya kuimba majukwaani tu bali kusimamia miiko na maadili ya chama na kuhakikisha tunaisimamia serikali kutekeleza miradi Kwa masilahi mapana ya wananchi.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilayani humo Hassan Lyamba mafunzo hayo wayatumie Kwa namna walivyofundishwa ikiwa ni mara ya kwanza kutolewa Kwa viongozi hao.
“Chama cha mapinduzi kinaongozwa kwa kanuni hivyo semina ya leo itawasaidia viongozi hao kujua namna ya kufanya kazi zao ikiwemo kujua masuala ya itifaki katika chama”, amesema Lyamba.
Mmoja wa viongozi hao Judith Shola amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa kujuwa uzalendo wa kukitumikia chama pamoja na kuisemea serikali Kwa namna inavyotekeleza kuwaletea wananchi maendeleo.
Mafunzo hayo yametolea Kwa viongozi hao kutoka kata ya Kafule ,Ikinga, Malangali, Ngulugulu, Sange, Lubanda ,kalembo na Luswisi.