Home KITAIFA CCM ILEJE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAENDELEO KWA WANANCHI

CCM ILEJE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAENDELEO KWA WANANCHI

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ileje Ndugu Patrick Ghambi ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan Suluhu kwa miradi mikubwa ambayo ameweletea wananchi wilaya ya Ileje katika kutatua changamoto zinazo ikabili jamii wilaya hapa.

Ghambi amesema kuwa katika kipindi ambacho Rais ameingia madarakani amefanya mambo makubwa katika wilaya ya Ileje ambapo ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kafule na ujenzi wa mradi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 900, barabara kwa kiwango cha lami kutoka kata ya Isongole mpaka Kasumulu wilaya ya kyela Mkoa wa Mbeya ambapo amedai kuwa miradi hiyo imelenga kutatua kero za wananchi .

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ileje Ndugu Hassan lyamba amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii kila mmoja kuhakisha anatimiza wajibu wake Ili kujipatia kipato cha kujikwamu na umaskini na kudai kuwa serikali ipo pamoja na wananchi katika kusogeza huduma karibu na wananchi ambapo amesema kuwa mwaka huu pembejeo za kilimo kama mbolea zitapatikana kwenye ofisi za kata wilayani hapa.

Naye Mbunge wa jimbo la Ileje na Naibu waziri wa ujenzi Mhe Eng. Godfrey Kasekenya Msongwe amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabili Wilaya ya Ileje ni miundombinu ya barabara ambayo amedai kuwa huwezi kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja bila kuwa na miundo mbinu bora ya barabara na kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya katika kufungua Ileje kwenye barabara mbalimbali zinazoendelea kujengwa katika wilaya ya Ileje na kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi katika masuala ya maendeleo na kuwatumia vizuri waatalamu wa serikali kuanzi ngazi za chini mpaka Taifa.

Aidha wajumbe wa kamati ya siasa wa CCM wilaya ya Ileje wameanza ziara ya kuwatembelea wanachama ngazi ya kata na kuzungumza nao pamoja na kukagua uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi wa maeneo husika.

Previous articleTANWAT WAPEWA SIKU 30 KUONDOA MITI KWENYE VYANZO VYA MAJI
Next articleTANZANIA NA MALAWI WAJADILI MRADI WA UMEME MTO SONGWE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here