Home KITAIFA CANADA WATOA DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MRADI WA KILA BINTI...

CANADA WATOA DOLA MILIONI 50 KWA AJILI YA MRADI WA KILA BINTI ASOME NA MPANGO WA AJIRA (UFUNDI STADI)

Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Canada imefadhili mradi wa “Kila Binti Asome” na mradi wa uwezeshwaji kupitia Program za ujuzi utakaogharimu Dola za Canada Milioni 50 kwa Shirika la UNICEF.

Mradi huo wa kila Binti Asome unaolenga kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania kukuza uwezeshwaji wake na kupata fursa za ajira staha, itachangia kuongeza viwango vya uhitimu kwa wasichana katika shule za sekondari.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa na Waziri mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki la Canada, Mhe.Harjit Sajjan, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Pamoja na mambo mengine ziara hiyo inayolenga kutembelea miradi ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Canada, amesema wote wanafahamu changamoto za kujifunza na kukuza ujuzi zinazowakabili mabinti wa Tanzania Bara na Zanzibar.

CHAMNGAMOTO ZINAZOWAKABILI MABINTI.

Akizungumzia changamoto za kujifunza na kukuza ujuzi zinazowakabili mabinti wa Tanzania Bara na Zanzibar, Sajjan amezitaja kuwa ni pamoja na tofauti za kimuundo, mzigo wa kazi za nyumbani na majukumu ya uangalizi wa familia, ukatili wa kijinsia.

Nyingine ni mitazamo na desturi za kimila, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, pale elimu ya wasichana inapochukuliwa kuwa ya thamani ndogo, hakuna motisha kwao kumaliza masomo, Kwa kuongeza, ni ukweli kwamba shule nyingi hazikidhi mahitaji ya wasichana walio katika kipindi cha balehe.

Waziri huyo alizitaja changamoto nyingine kuwa ni, si kwa suala la usalama, au upatikanaji wa Maji au vyoo Maalum vya kuhifadhi wakati wa hedhi, wasichana wote wanapaswa kupata fursa ya elimu na wasichana wote wanapaswa kupata fursa ya kumaliza masomo yao bila kujali hali zao.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake kuwezesha upatikanaji wa elimu, tunawapongeza kwa maendeleo makubwa katika ngazi ya elimu ya msingi ambapo usawa wa kijinsia umefanikiwa, tunampongeza juhudi za kuondoka marufuku ya mabinti wenye ujauzito na mabinti waliojifungua kurejea shuleni,”amesema Sajjan

Previous articleKIINI UKOSEFU WA HAKI KWA WALEMAVU CHATAJWA
Next articleNDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI BAADA YA KULAZIMIKA KUTUA KWA DHARURA UWANJA WA NDEGE MANISPAA YA BUKOBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here