Home KITAIFA C-SEMA YA WAKUTANISHA KENYA NA TANZANIA KUJADILI MASWALA YA UKEKETAJI

C-SEMA YA WAKUTANISHA KENYA NA TANZANIA KUJADILI MASWALA YA UKEKETAJI

Shirika la C-SEMA kwa Ufadhili wa UNFPA limewakutanisha wadau kutoka na Tanzania na Kenya kujadili namna Bora ya kukabiliana na vitendo vya ukeketaji huku wadau wakitaka kuelekeza nguvu Zaidi katika Kundi la watu wenye ulemavu ambalo nikama lilikuwa limesahaulika.

Akizungumza mkuu wa Miradi kutoka shirika la C-SEMA Michael Marwa amesema Kundi hilo linapewa kipaumbele kwa sasa nakuhakikisha watoto wakike wenye ulemavu wanakuwa salama.

“Tunaandaa mikakati ambayo tunahakikisha wenzetu wenye ulemavu wanakuwa salama nakuhakikisha inavotokea wanataka kukeketwa tunawaoko lakini pia kuwasaidia wanapohitaji msaada kwahiyo tunaweka mipango ambayo tunauhakika utawasaidia kuepukana na vitendo hivyo”Michael Marwa mkuu wa Miradi C-SEMA.

Kwa upande mkuu wa Wilaya ya Mabela Nchini Kenya Joyfillah Wambua amepongeza shirika la C-SEMA kuja na mpango wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu wakike kuepukana na vitendo vya ukeketaji Kwani itasaidia sasa kuwasaidia Kwa kiasi kikubwa Kwan wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na kutokuwa na Uwezo wa kujitetea.

“Hakikisheni mnaiomba serikali pia inaweka miundombinu wezeshi kwa watu wenye ulemavu wasipate changamoto ya huduma katika maeneo yao kwahiyo niwakati wakuwasaidia kwa Tanzania na hata kwa Kenya nahili limekuwa likifanyika vyema”Alisema Joyfillah Wambua Mkuu wa Wilaya Mabera Nchini Kenya.

Kwa upande wake Godfrey Juma ambae nikijana mwenye ulemavu amesema atakuwa baloz mkubwa katika Kundi hilo kwani imemsadia Kupata Elimu ambayo ataifikisha kwa jamii hiyo ili ifaham na man yakuniokoa yanapotokea Matukio ya ukeketaji huku akiomba serikali kuwepo kwa uwezesho mkubwa katika kundi hilo.

Previous articleWIZARA YA MADINI YASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA SERIKALI YA URUSI NA NCHI ZA AFRIKA
Next articleMAMA ADAIWA KUUA KICHANGA, AZIKA KICHWA PEKEE _ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JULAI 29/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here