Bweni la Wanafunzi 64 katika Shule ya Sekondari Vwawa iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe limeteketea kwa moto leo Aprili 14/2023 na kuteketeza vitu vilivyokuwa ndani.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Songwe, Elautery Mremi amesema moto huo umeanza leo asubuhi ambapo Jeshi hilo limefanikiwa kuudhibiti usienee kwenye mabweni mengine na madarasa nakusema kuwa hakuna majeraha wala vifo vilivyosababishwa na moto huo huku tathmini ikiendelea kubaini madhara na chanzo cha moto huo.
Kamanda Mremi amesema bweni hilo lilikuwa linatumiwa na Wanafunzi 64 ambapo vitu vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo vimeteketea, wakati moto huo unatokea Wanafunzi walikuwa darasani wakiendelea na mitihani.
Hatahivyo mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.