Bunge limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na 3 wa Mwaka 2023 unaopendekeza kufanya marekebisho katika Sheria Mbili zinazohusu uwekezaji utakaosaidia utekelezaji Bora wa Sheria hizo na kuboresha ufanisi wa majukumu ya Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.
Akiwasilisha Muswada huo BungeniĀ Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt Elieza Feleshi amesema marekebisho hayo yamezingatia haki idhini ya utendaji wa Majukumu ya Mawaziri wenye Dhambana tofauti na ilivyokuwa.
Amesema kwa sasa Sheria hizo zimamtafsiri Waziri Mwenye Dhamana kama Waziri wa Viwanda ilihali Jukumu la Usimamizi wa Maswala ya uwekezaji limehamishiwa wizara ya Mipango na uwekezaji.
Baadhi ya wabunge waliochangia muswada huo wa marekebisho ya sheria mbalimbali akiwemk mbunge wa jimbo la Mlalo ( CCM) Rashid Shangazi wamesema marekebisho hayo yatasaidia kuongeza kasi ya uwajibikaji na mabadiliko ya kiutendaji wa Serikali.
..