Mashindano ya Bulaya Cup yanatarajiwa kuanza kutimua Vumbi leo Oktoba Mosi,2023 katika viwanja mbalimbali wilayani Bunda mkoani Mara huku mashindano hayo yakishirikisha timu 22.
Mshindi wa kwanza wa mashindano haya ataibuka na kiasi cha shilingi Milioni 2 mshindi wa pili milioni 1 huku mshindi wa tatu atajinyakulia laki 5.
Akikabidhi jezi mwandaaji wa mashindano hayo Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya amesema mashindano hayo yanalenga kwenda kuibua vipaji ambavyo viko katika wilaya kama ilivyo kawaida yake.
“Mashindano haya yamewaibua akina Sixtus Sabilo pamoja na kina majogoro ni wakati sasa wakuangalia vipaji vingine wameniomba nami nimeitika.
Mashindano hayo yatagusa michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguuu wanawake Mpira wa miguuu wanaume,Pete,Bao ,pooltable n.k huku Fedha ya mashindano yote ikigharimu kiasi cha shilingi Milioni 20