Home KITAIFA BODI 55 ZA VYAMA VYA USHIRIKA VILIVUNJWA NA TCDC 2022/2023

BODI 55 ZA VYAMA VYA USHIRIKA VILIVUNJWA NA TCDC 2022/2023

 

Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)DKT. Benson Ndiege amesema Katika kipindi cha Mwaka 2022/2023, Tume hiyo ilifanya ukaguzi kwenye Vyama vya Ushirika na jumla ya 4,712 vilibainika kuwa na mapungufu mbalimbali ya kiutendaji, ikiwemo urasimishaji wa mali za vyama , utunzaji wa nyarakannaa kumbukumbu nyingine za vyama na mapungufu hayo yalifanyiwa kazi kwa kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu.

 

Akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji na Vipaumbele vya Tume hiyo kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Agosti 11,2023 jijini Dodoma Dkt.Ndiege amesema hatua zilizochukuliwa ni kuvunja bodi 55 za Vyama vya Ushirika, kupeleka masuala 30 polisi na masuala 47 yanashughulikiwa na TAKUKURU pamoja na kutoa mafunzo kwa watendaji 4,732 wa Vyama vya Ushirika.

 

Amesema kuwa Hadi kufikia Juni 30, 2023, jumla ya kilo 1,826,850,970 sawa na tani 1,826,850.97 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.75 ziliuzwa kutoka kwenye mazao ya tumbaku, korosho, pamba, kahawa, ufuta, kakao, mkonge, chai, mbaazi, soya, zabibu, miwa na maharage.

”jumla ya kilo 1,826,850,970 sawa na tani 1,826,850.97 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.75 ziliuzwa kutoka kwenye mazao ya tumbaku, korosho, pamba, kahawa, ufuta, kakao, mkonge, chai, mbaazi, soya, zabibu, miwa na maharage.”amesema Dkt Ndiege.

Mbali na hayo amesema katika kutekeleza majukumu ya tume hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tume hiyo inafanya mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata Mikopo yenye Riba nafuu na kufikia Disemba 2024, Tume itakuwa imeshazindua Benki ya Taifa ya Ushirika (KCBL) na kuwa mali ya wanachama katika kujipatia mikopo ya kuendesha shughuli zao kikamilifu.

Hata hivyo dkt. Ndiege ameeendelea kwa kusema tume kwa kushirikiana na mamlaka ya serikali mtandao (eGA) Imetengenenza mfumo wa kidigitall wa usimaminzi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) , unaolenga kurahisisha usimaminzi wa uendeshaji wa vyama vya ushirika kwa nia ya kuongeza ufanisi , uwazi na uwajibilaji.

Previous articleDAWA HII ITAKUSAIDIA KUONGEZWA MSHAHARA KAZINI
Next articleTANZANIA NA MALAWI ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA NISHATI, KUANZA NA MRADI WA UMEME WA MTO SONGWE (MW 180)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here