Home KITAIFA BODABODA WASHAURIWA KUACHA TAMAA ZA KIMWILI ILI KUTIMIZA MALENGO YAO

BODABODA WASHAURIWA KUACHA TAMAA ZA KIMWILI ILI KUTIMIZA MALENGO YAO

 

NA ENEA MWANJA, MBOZI SONGWE.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Esther Mahawe, amewataka Madereva wa Pikipiki maarufu Bodaboda kuweka mipango ya maendeleo na kutulia na wake zao badala ya kuhangaika na wanawake wanaoonekana kuwa wazuri mtaani huku wakiwaacha wake zao.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye semina ya madereva hao iliyofanyika katika ukumbi wa Polisi mjini Vwawa Wilayani Mbozi.

Bi. Mahawe amesema kuwa ili Madereva hao wapate maendeleo ni lazima kuweka mipango mizuri ya fedha na si kuzitumia katika mambo ya anasa.

“Unakutana na demu mkali anapita temana naye yaani fanya hujaona, si yupo mama (Mke) kule nyumbani? Eee achana na hizi mambo sio unatamani nyama choma na bia, hii hela yangu itanunua mfuko wa Simenti. Kwa hiyo lazima muwe na malengo. Watanzania wengi tunafeli kwa sababu hatuna malengo”, amesema kwa msisitizo Dc Ester Mahawe na kuongeza.

“Kama huna malengo hata nikikupa milioni 10 saa hizi utaona umepata bonge la bingo halafu utaenda utanunua jinsi mpya na kutafuta demu mkali uende naye Mbeya, si haujapangilia. Lakini kama ungekuwa na malengo ikitokea hiyo si ni fursa hiyo? sasa nendeni mkatekeleze njozi zenu”, amesema Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Previous articleUWT KATA YA ZIWANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU
Next articleHOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YABUNI NA KUTENGENEZA GARI MAALUM LA KUBEBA WAGONJWA NDANI YA HOSPITALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here