Home KITAIFA BILIONI 41.2 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA UFUTA PWANI

BILIONI 41.2 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA UFUTA PWANI

Shilingi bilioni 41.2 zimelipwa kwa wakulima wa ufuta katika mkoa wa Pwani baada ya mauzo ya tani 13. 6 katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/2023 Ambapo tayari minada sita imeshafanyika mkoani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani Meneja wa Chama kikuu Cha Ushirika Cha wakulima mkoa wa Pwani CORECU Mantawela Hamisi amesema fedha zote zimekwishalipwa kwa Wakulima na wadau wake wakiwemo Halmashauri na Taasisi zinazohusika katika mnyololo wa kuongezea thamani mazao.

Amesema minada hiyo sita iliyofanyika ni kutokana na mavuno ya mpando wa kwanza ambapo Sasa mavuno ya mpando wa pili inatarajiwa kuanza ambapo minada 4 inatarajiwa kufanyika.

Aidha Mantawela amewataka wakulima kuzingatia kulinda ubora wa zao hilo la Ufuta ikiwa ni pamoja na kusafisha ufuta wao kabla ya kupeleka kwenye vyama vya Msingi tayari kwa mauzo.

Previous articleKOCHA WA MANCHESTER UNITED AELEZA KWANINI ALIMCHAGUA ANDRE ONANA
Next articleMALUMBANO YA BANDARI YAMCHEFUA ASKOFU_ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JULAI 22/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here