Home KITAIFA BENKI YA NBC KWA KUSHIRIKIANA NA TFF WAMETAMBULISHA CHAPA MPYA YA LIGI...

BENKI YA NBC KWA KUSHIRIKIANA NA TFF WAMETAMBULISHA CHAPA MPYA YA LIGI YA CHAMPIONSHIP 2023/24

Na Dishon Linus

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imezindua rasmi chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwa sasa inafahamika kwa jina la NBC Championship hatua ambayo imekwenda sambamba na uzinduzi wa mashindano hayo ya soka yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ujio wa chapa hii ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba wa udhamini tuliosaini hivi karibuni baina yetu unaotupa fursa ya kuendelea na udhamini wa kwenye ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara ‘NBC Premier League’ hadi msimu wa 2027/28.

Mkataba huo wenye thamani ya TZS 32.56 bilioni pia unajumuisha ligi za vijana kwa klabu zinazoshiriki ligi kuu ‘NBC Youth League’ na ligi ya daraja la kwanza “NBC Championship”.

Tukio la uzinduaji wa chapa hii mpya umefanyika leo Makao Makuu ya NBC jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi waandamizi na wadau wengine wa mchezo wa mpira wa miguu wakiwemo waandishi na wachambuzi.

Kwa upande wa mkurugenzi wa wateja binafsi kutoka NBC ndugu Elibariki Masuke alisema. “Leo hii tuko hapa kutimiza sehemu ya jukumu letu la kimkataba na udhamini kuzindua chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) na kuipa jina la NBC Championship League (NBC Championship) kama sehemu ya uzinduzi wa mashindano haya ya soka yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.”

Ikumbukwe ligi ya championship inaanza tarehe 9 mwezi wa 9 Kwa baadhi ya michezo kuanza kutimua vumbi katika viwanja mbali mbali huku malengo ya kila timu ni kufanya vizuri ili kuweza kufanikiwa kupanda ligi kuu Tanzania bara.

Previous articleKATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA MRADI WA JNHPP, ASEMA WATANZANIA WANAHITAJI UMEME
Next articleMAJALIWA AMWAGIZA DKT. BITEKO KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAFUTA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here