Na Theophilida Felician Kagera.
Umoja wa baraza la wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema BAWACHA Mkoa Kagera umekutana pamoja kwenye kikao na kuzungumzia mambo kadha wa kadha ya chama ikiwemo ya kutoa tamko la ufafanuzi wa kauli za Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi UWT taifa Mhe Mery Chatanda ambazo amekuwa akizitoa zikimlenga moja kwa moja mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freemani Aikaeli Mbowe.
Akifafanua kwa undani kauli hizo mbele ya wanawake wa BAWACHA Kagera kutoka majimbo yote 9 ya uchaguzi Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa Kagera Mhe Pendo Luis Ngonyani ameeleza kuwa Mery Chatanda amekuwa akitoa kauli tofauti tofauti dhidi ya Mwenyekiti Freemani Mbowe kupitia njia mbali mbali ikiwemo ya vyombo vya habari na mikutano ya hadhara.
“Mwenyekiti wa UWT taifa Mery Chatanda alisikika kwenye vyombo vya habari kadhaa akitoa kauli za kumuataki Mwenyekiti wetu wa chama Taifa Mhe Mbowe sasa hatuwezi kukubali kuona Mwenyekiti wetu anaatakiwa sisi kama baraza tukakaa kimya haiwezikani” amesema Mwenyekiti Pendo Ngonyani Mbele ya wanawake katika kikao hicho kilichowakutanisha Manispaa ya bukoba
Mwenyekiti huyo ametolea mfano wa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na kiongozi huyo ni pamoja na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Mkoani Lindi tarehe 16 /7/2023….
“alitoa kauli hivi ni kwamba mhe Mbowe hana Shukrani na mnukuu Mery Chatanda alisema Mbowe aliwekwa ndani na Rais Magufuli Rais Samia akamtoa naomba nimkosowe Mwenyekiti wa UWT Tanzania ni hivi na mkumbusha aliyemuweka ndani Mwenyekiti Mbowe ni Rais Samia nasiyo Rais Magufuli Mwenyekiti wetu alikamatwa Tarehe 20/7 2021 akiwa Mwanza ikiwa ni miezi minne baada kutokea kifo cha Magufuli kwa hiyo suala la kubambikiziwa kesi ya ugaidi Mwenyekiti wetu halikuwa la Magufuli bali lilikuwa ni la Rais Samia” ameeleza bayana Pendo Ngonyani.
Kauli nyingine alizozitoa ambazo zimekuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa UWT dhidi ya Mbowe ni pamoja na nakusema kuwa Mwenyekiti Mbowe amekuwa akituhumu kuuzwa kwa bandari ya dar kwenye kampuni ya Dp Waorld.
Ufafanuzi kuhusu suala la bandari kwa pamoja wanawake hao wamebainisha kuwa wanapinga vikali mkataba wa bandari hiyo kwani una mapungufu kadhaa maana hauonyeshi ukomo wala hauonyeshi watawekeza kiasi gani nataifa litapata kiasi gani.
Hata hivyo Ngonyani amegusia suala la madai ya Katiba mpya jinsi linavyoendelea kufanyiwa kazi kwa malengo ya kufanikiwa zaidi ili kuhakikisha katiba mpya inapatikana kwa wakati na sivinginevyo.
Ameongeza kusema kuwa kwa sasa chama cha Chadema Taifa kipo ukanda wa ziwa Victoria kwa ajili ya shughuli mbalimbali za chama ambapo tarehe 28/7 mwaka huu wa 2023 Viongozi wa chama hicho Taifa watakuwa Kagera ili kukutana na wananchi wa Mkoa huo.