Mbunge wa Jimbo la Ileje na Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mhe. Godfrey Kasekenya Msongwe jana alifanya ziara katika kata ya Kalembo katika kijiji cha Mbangala na kufatiwa na mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kijiji cha Kalembo
Akiwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalembo Mhe. Kasekenya aliweza kuzungumzia swala la bandari na kusema
“Bandari yetu haijauzwa ila kinachofanyika ni uwekezaji ambapo kwa sasa tunaingiza tirioni 6 kwa mwaka itapanda mpaka kuwa tirioni 26 kwa mwaka”
Mhe. Kasekenya pia alisikiliza kero za wananchi na kuzitolea ufafanuzi. Moja ya kero iliyowasilishwa ni kukosekana sehemu ya kulala ndugu ambao hupeleka wagonjwa katika hospital ya Wilaya ya Ileje
Akiwa katika Kijiji cha Mbangala Mhe. Kasekenya alikagua miundombinu ya shule na barabara pamoja na msingi wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji inayojengwa na Wananchi na kuchangia shilingi laki 2
Ndugu. Jackson Mbuba mwenyekiti wa Tawi la CCM Mbangala alisema amefurahishwa na ujio wa mbunge na kumuomba alitazame swala la barabara kwani imekuwa changamoto kubwa katika Kijiji hicho