Leo tarehe 19 Novemba 2023, Balozi wa Tanzania Nchini Algeria Iman Njalikai amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu Jaji Iman Aboud, katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Algiers.
Jaji Aboud anaongoza mkutano wa 71 wa mahakama hiyo unaofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria kuanzia tarehe 06 Novemba 2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 04 Desemba 2023.
Mkutano huo, utakapokamilika unatarajiwa kutoa hukumu ya mashauri takriban 9 ya kimahakama.