Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Kilimanjaro wanatarajia kufanya maandamano ya amani ya kupinga Vitendo vya Ushoga ambavyo vimeonekana kushamiri duniani kote.
Hayo yameelezwa na Shekhe wa Mkoa wa Kilimanjaro Shabani Mlewa April 4 2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Baraza hilo Mkoani Kilimanjaro.
Mlewa amesema maandamano yatashirikisha watu kutoka dini mbalimbali na kuwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki ili kutoa ujumbe kwa mataifa mbalimbali kuwa Nchi ya Tanzania haikubali Vitendo hivyo.
Maandamono hayo yanatarajia kufanyika April 08.2023 na yakianzia katika viwanja vya Ofisi za BAKWATA Kilimanjaro na yataishia katika viwanja vya mashujaa Mkoani humo.