Sio tu kutumia lugha ya Kiswahili na ki-Yoruba kwenye ngoma yake ya ’LabaLaba’ inayomaanisha Kipepeo, ngoma ambayo inamahadhi ya Amapiano, aliyomshirikisha DJ Latitude na Iam Beatz , Ayanfe anatarajia kufanya mapinduzi makubwa ya muziki kwa kufanya Tour katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ikijumuisha nchi kama Tanzania, Kenya na Uganda.
Ayanfe ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa kurekodi na ALPHA NATION anatarajiwa pia kutoa EP. Na tayari ameshafanya kazi na wasanii wa kubwa kutoka Nigeria hasa kutoka lebo ya DMW ya Davido ambapo miaka miwili iliyopita alifanya kazi na Mayorkun iitwayo WHAT’S GOIN ON na mwaka 2022 akaachia ngoma na Davido iitwayo MIGRATE .
Ayanfe amewataka mashabiki zake kutarajia mambo mazuri kama kupata kolabo za utofauti ambapo amesema hatoufunga mwaka 2023 bila kuwapatia kolabo safi na wasanii pendwa wa Afrika Mashariki.