WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,amekemea tabia ya baadhi ya watendaji katika Sekta ya Maji kutotimiza majukumu yao ipasavyo na badala yake wamekuwa wakitoa visingizio visitvyo na msingi kwani vinarudisha nyuma maendeleo.
Pia amesema hatosita kuchuwachukulia hatua kwa watakaobainika kutotimiza majukumu yao.
Waziri Aweso ametoa Kauli Juni 27,2023 Jijini Dodoma wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Nadhifa Kemikimba amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji hasa Vijijini lakini watahakikisha wanaitatua changamoto hiyo.
Akitoa maelezo kuhusiana na Mfuko wa Taifa wa Maji,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,Haji Nandule amesema kuwa Mfuko umekusanya jumla yaShilingi Bilioni 284.6 na kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Maji wa Taifa Abdallah Mkufunzi ameahidi kutekeleza majukumu ya mfuko huo kwa uadilifu kwakuzingatia KanuniI,taratibu na miongozo.