Home KITAIFA ANDIKENI WOSIA ILI KUEPUSHA MIGOGORO

ANDIKENI WOSIA ILI KUEPUSHA MIGOGORO

 

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka watanzania kujijengea utamaduni wa kuandika wosia mapema kabla hawajafariki ili kuepusha migogoro ya kifamilia inayotokea pindi mwanafamilia anapofariki na kuacha imani kuwa kuandika wosia ni kujitabiria kifo.

Amesema baadhi ya migogoro mingi ya mirathi inatokana na watu wengi kutokuandika wosia wakiwa hai ambapo ameielekeza wizara ya katiba nasheria na ofisi ya kukabidhi wasii kutoa elimu kuhusu uandaaji wa wosia na masuala ya mirathi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema kampeni hiyo inapaswa kutoa elimu ya kutosha kuhusu taratibu za kufuata ili kupata haki na itoe kipaumbele katika kutoa elimu kuhusu haki za watu wenye ulemavu.

Nae Waziri wa Katiba wa Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ni mkakati unaotekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wenye lengo la kuongeza uelewa wa sheria na haki za binadamu kwa Wananchi wote hususani Wanawake, Watoto na makundi maalum.

Previous articleSHULE YA MWALIMU NYERERE YAWAFUNDA VIONGOZI WANAWAKE WA TAASISI NCHINI
Next articleWAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO MKUBWA WA ASKARI POLISI WA KIKE DUNIANIĀ 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here