Mwanaume mmoja nchini Korea Kusini amekamatwa baada ya kufungua mlango wa dharura wa ndege ya Shirika la Asiana ilipokuwa ikiwasili nchini Korea Kusini ikiwa bado umbali wa mita 250.
Ndege hiyo iliyowasili katika uwanja wa ndege wa kimataufa wa Daegu katika mji wa Gyeongsang – do ikitokea katika kisiwa cha Jeju nchini Korea Kusini ilikuwa imebeba abiria 194 ambao wote walisalimika baada ya tukio hilo.
Baadhi ya abiria walikimbizwa hospitalini baada ya kupoteza fahamu na wengine kupata matatizo ya kupumua.