Home KITAIFA AJALI YAUA RAIA SITA WA KIGENI NJOMBE

AJALI YAUA RAIA SITA WA KIGENI NJOMBE

Njombe

Polisi mkoa wa njombe wanamsaka Dereva na kondakta wa gari aina ya Scania yenye namba za usajili T.501 AGJ waliosababisha ajali eneo la Iyai na kupelekea vifo vya watu sita na majeruhi nane wote Raia wa kigeni wakisadikika kuwa ni kutoka Ethiopia.

Akizungumza katika eneo la tukio kamishna msaidizi wa Polisi John Makuri Imori amesema ajali hiyo imetokea mapema alfajiri ya kuamkia hii leo, huku watu sita raia wa kigeni, wakiripotiwa kufariki dunia na wengine nane wakiwa majeruhi, ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya wanging’ombe.

“Aajali hii ilihusisha gari namba T 501 AGJ aina ya Scania iliyokuwa na tela lake lenye namba T595 ANJ iliyokuwa inatoka Makambako kuelekea Zambia baada ya kufika hapa tumekuta ndani ya gari kuna mizigo mingi sana ya vifaa vya ujenzi lakini pia baada ya kufungua tela tumekuta watu ambao ni raia wa kigeni na bahati mbaya hatujapata hati zao zozote za kuwatambulisha”amesema Kmanda Makuri.

Bado raia hao hawajabainika wazi ni kutoka nchi gani, licha ya kwamba taarifa za awali zinabainisha kuwa ni raia wa ethiopia.

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Cloudia Kita ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa bin adamu.

Previous articleRC GEITA ATOA MAAGIZO KWA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA DHAHABU KUWALIPA WANANCHI FIDIA KWA WAKATI
Next articleBEBA ABIRIA KULINGANA NA IDADI ILIYOELEKEZWA KWENYE GARI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here