Mtu mmoja amefariki dunia na nane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwepo basi la abiria lilikuwa likitokea Musoma kuelekekea Dar-es-salaam katika eneo la Kingolwira Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya kuelekea Dar-es-salaam .
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo ikihusisha lori lenye namba za usajili T 960 DSV na basi kampuni ya Johanvia lenye namba za usajili T 728 EBT lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Dar-es-salaam kugongana na gari la polisi .
Kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro Abilahi Issa ,amekiri kupokea kwa mwili huo uliotambulika kwa majina ya Yohana Nathani pamoja na majeruhi nane ambao wanapatiwa matibabu katika hospital hiyo,ambapo watano ni jinsia ya kiume na watatu ni jinsia ya kike.