Home KITAIFA AGIZO LA RC HOMERA BADO GIZA KUFUNGULIWA SOKO LA TUNDUMA

AGIZO LA RC HOMERA BADO GIZA KUFUNGULIWA SOKO LA TUNDUMA

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya vijijini (kichama) imeagiza kufunguliwa kwa Soko la Tunduma Road Kata ya Nsalala Wilayani Mbeya kwani soko hilo lilishakamilika lakini halijaanza kufanya kazi hadi sasa licha ya mkuu wa mkoa kuagiza lifunguliwe kufikia mwanzoni mwa mwezi wa sita.

Hayo yamejiri baada ya Kamati ya Siasa ya CCM wilayani Mbeya vijijini kutembelea na kukagua soko hilo ambalo kero kubwa hata kutofunguliwa kwa soko ni ufinyu wa barabara ambapo wajumbe wa Kamati ya siasa walitoa maoni mbalimbali ya kuharakisha ufunguzi soko hilo ili kuiingizia mapato Serikali.

Alipopewa nafasi ya kueleza mkakati wa kupanuliwa kwa barabara hiyo Meneja wa Wakala wa barabara vijijini Tarura wilaya ya Mbeya mhandisi Selemani Mziray amesema kikwazo kikubwa ni ufinyu wa bajeti na kutokuwepo kwa bajeti juu ya ujenzi unaohitajika kutoka barabara kuu hadi sokoni Nsalala hususani upatikanaji wa kifusi kinachohitaji zaidi ya Mil.miamoja.

Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Mwalupindi ameagiza soko hilo kufunguliwa wakati miundombinu mingine ikiendelea kurekebishwa hususani utafutaji fedha za ujenzi barabara hiyo.

Wafanyabiashara wa Nsalala mjini humo wanasema kufunguliwa kwa soko hilo kutawasaidia kiuchumi na kuinua uchumi wa Serikali..

Previous articleMKATABA DPW NI KITANZI, NASHAURI URUDI BUNGENI, WANANCHI WASHIRIKISHWE: MGOMBEA UBUNGE BUSOKELO
Next articleVIJANA 50 WAPEWA MAFUNZO YA KUDUMISHA AMANI MKOANI MTWARA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here