Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema Migogoro ya kiutawala inayoendelea kwa baadhi ya Ofisi za Umma husababisha ucheleweshwaji wa maendeleo hali ambayo inawanyima wananchi haki yao ya msingi na wengine kuichukia serikali kwa makosa ya watu wachache wasio waadilifu kazini.
Kauli hiyo imetolewa Juni 4, 2023 Jijini Dodoma Wakati Wa mafunzo elekezi ya uongozi kwa Makatibu Tawala na Wilaya Tanzania Bara huku akiwanyooshea vidole baadhi ya watendaji wa serikali kuwa vinara wa utovu wa nidhamu.
Pia Waziri Mkuu Majaliwa amewaonya watendaji wa Serikali kuacha mihemko yakujibizana kwani kwa kufanya hivyo inapelekea majibishano ambayo yanawezankutoa siri za Serikali.
Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao na wanapobaini kuwepo kwa ubadhilifu wasisite kuchukua hatua.
Majaliwa amesema ili viongozi hao waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo wanatakiwa waweke mikakati namba ambavyo wilaya zao ya zitakavyoweza wilaya kubeba na kusimamia vizuri ajenda za kitaifa.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Angela Kairuki ameonyesha kukerwa na vikao vya usuluhishi wa migongano ya kazi kwa baadhi ya watendaji huku akiagiza ziara zinazofanywa na watendaji ziwe na matokeo chanya na waache kufanya ziara kama matembezi binafsi.
Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete alitoa wito kwa viongozi hao wahakikishe mafunzo wanayopatiwa wanakwenda kuyafanyia kazi katika maeneo yao.
Makatibu Tawala na Wilaya Tanzania Bara takribani 135 kati ya 139 ambao hawajafika wanasababu mbalimbali.